Kwa watu wengine, hii ni diplomasia ya kawaida viongozi wa nchi tofauti wakikutana katika mkutano wa kimataifa. Lakini kwa wengi, picha hiyo ni ishara ya mchanganyiko mkubwa: wakati mabomu yanadondoka katika Rutshuru, wakati mamilioni ya raia wa Congo wanakimbia makazi yao mashariki, wawakilishi wa taasisi za kisiasa wanakaa pamoja kwa utulivu katika majukwaa ya kimataifa.
Diplomasia ya Tabasamu Katika Wakati wa Machungu
Katika hotuba yake mbele ya APF, Vital Kamerhe alisisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa mataifa, kudumisha demokrasia na kuhakikisha amani ya kudumu kwa nchi za Francophonie. Ingawa hakutaja Rwanda, ujumbe wake ulikuwa wazi kwa kila mtu anayefahamu hali ya mashariki mwa Congo.
Kwa upande wake, Mussa Fazil Harerimana alizungumza kuhusu ushirikiano wa kikanda na maendeleo, akiepuka kabisa mada yoyote ya kisiasa au migogoro ya sasa. Ukimya wake umefasiriwa na wachambuzi kama ishara ya msimamo wa Kigali: kutotaka kujihusisha moja kwa moja, lakini kuendelea kushikilia msimamo wake kupitia njia nyingine.
Siasa za Ndani Zajikuta Katika Mtego wa Maadili na Realpolitik
Kwa upande wa nyumbani, hasa katika duru za kisiasa za Congo, tukio hili limepokewa kwa mchanganiko wa hisia. Wengine wanamshutumu Vital Kamerhe kwa kutoa ishara ya kukubaliana kimya kimya na serikali ya Rwanda, wakati wengine wanamtetea kuwa ni sehemu ya diplomasia ya lazima ya kuokoa ushirikiano wa kikanda.
Ni wazi kuwa Kamerhe anatembea kwenye kamba nyembamba: kuwa mwanasiasa wa kitaifa anayehubiri umoja wa kitaifa, huku akiwa pia mshiriki wa majukwaa ya kimataifa yanayomkutanisha na wale wanaotuhumiwa kuunga mkono waasi wa M23.
Uhusiano Wa Kushangaza: Kutegemeana Katikati ya Vita
Licha ya migogoro ya mara kwa mara, Rwanda na Congo zinaendelea kuwa na uhusiano wa karibu katika biashara, usafiri, na hata urasimu wa kikanda. Maelfu ya raia hupita mipakani kila siku kati ya Goma na Rubavu, na bidhaa hutoka upande mmoja kwenda mwingine — hata wakati majeshi yao yanakabiliana mashambani.
Hali hii ya mkachanyiko inazua swali: je, uhusiano huu unaweza kuwa mzuri au ndio chanzo cha majeraha yasiyoisha?
Wakati mkutano wa APF ukiendelea katika utulivu wa Kanada, raia wa Congo mashariki wanaendelea kukumbwa na mashambulizi, njaa na hofu ya siku zijazo. Na huku viongozi wakitoa hotuba nzuri mbele ya kamera, hali halisi bado ni ya majonzi.
Hii ndiyo maana wachambuzi wengi wanasema: uhusiano