Ingawa kiatu hicho hakikumpata Rais Ruto, tukio hilo lilisababisha mchanganyiko wa muda mfupi, liki wazalimisha maafisa wa usalama wa rais kuchukua hatua za haraka kumlinda kiongozi huyo wa taifa. Mshukiwa huyo alikamatwa papo hapo na kuondolewa eneo hilo chini ya ulinzi mkali.
Licha ya tukio hilo la kushtua, Rais Ruto aliendelea na hotuba yake dakika chache baadaye, akionekana mtulivu huku akitumia fursa hiyo kusisitiza umuhimu wa uvumilivu wa kisiasa na kuheshimu maoni tofauti.
“Ningependa kuwaambia wananchi wenzangu kuwa tofauti zetu haziwezi kutupeleka kwenye chuki au dharau. Tujenge taifa letu kwa mazungumzo na kuheshimiana, siyo kwa matukio kama haya,” alisema rais kwa sauti thabiti, akishangiliwa na sehemu ya umati.
Mamlaka za usalama zimeripoti kuwa mtu aliyerusha kiatu anashikiliwa na Polisi kwa mahoji zaidi, huku uchunguzi wa kina ukiendelea kubaini nia yake. Taarifa za awali zinaashiria kuwa huenda tukio hilo lilikuwa la mtu binafsi asiye na uhusiano wa moja kwa moja na kikundi chochote cha kisiasa, lakini hii haijathibitishwa rasmi.
“Tunachunguza kwa kina ili kujua kama ilikuwa ni hatua ya kujieleza kisiasa, upinzani wa kisera, au jaribio la kuleta vurugu kwa makusudi.”
Tukio hilo limezua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wakilaani vikali kitendo hicho, huku wengine wakikitazama kama ishara ya hasira na kukata tamaa kwa baadhi ya wananchi dhidi ya hali ya kiuchumi na utawala wa sasa.
Vyama vya upinzani vimeelezea kusikitishwa kwao na tukio hilo huku vikisisitiza kwamba mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana kwa vitendo vya vurugu, bali kupitia mijadala ya wazi na demokrasia inayoendeshwa kwa amani.
Mashirika ya kiraia pia yametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kupunguza lugha za uchochezi, wakionya kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa yanahitaji busara na uongozi wa kuvumiliana.