Vitendo hivyo vya unyanyasi na vya uzuni kali vinakuwa vikiendeshwa zaidi na vikosi vya usalama ambavyo ni wanamemba wa kundi la waasi wa M23; kikundi ambacho kinakuwa, tangu myezi tatu leo kikiendesha sheriya Katika sehemu Mbalimbali za Jimbo la kivu kusini.
Katika mitaa zote tatu za Muji wa Bukavu ambamo wakaaji wanaishi kwa woga na kusulumiwa kiolela, mili bila uhaii zaonekana kila mara zikitupiliwa ndani ya mifereji, huku zikimaanisha ugeukaji Mrefu wa sheriya inchini na duniyani kuhusu ukingo wa Maisha ya kibinadamu.
Wakati njaa na mashambulizi vya zidishwa mahali popote, wakaaji wanakuwa wakishutumu vikosi askari wa M23 kuwa ni wao wenyeji wa hali hiyo mbaya na kulaumu vikali hali ambamo wakaaji wanakuwa wakiishi, siyo tu ukose wa chakula wala Amani, lakini tena, ukosefu wa waongezi Bora kati ya waasi wale ambao wanakuwa wakijiita kuwa viongizi wa Jimbo.
Kama vile huko Goma, jimboni Kivu la kaskazini ambako vitendo vya ubakaji vyakipotiwa kila siku, Bukavu nako, wamama hata wajawazito na mabinti ambao zaidi ni wanafunzi, wanakuwa kila siku wakikumbwa na hali za ubakaji bila sababu, wamoja wakiuwawa kisha vitendo hivyo vya ngono.
Hayo yote ni kwa sababu serkali ya kongo hayijawayi kufikiliya lengo lake la kuwalinda watu na Mali yao katika usalama bila shaka na bila uchaguzi.
Vijana piya wanakumbwa na hali hizo.
Wakizaniwa kuwa wenyi Nguvu zaidi na mashujaa bila kipimo, Vijana wengi wanakuwa wakitekwa nyara siku kwa siku, wengi wakishutumiwa kuwa Na mahusiyano na uongozi wa Kinshasa huko Léopoldville, ambako viongizi wengi toka Jimbo la Kivu kusini walijielekeza kwa kuepuka magonvi na waasi, wengine waki fitiniwa bure mpaka kutendewa vitendo hivyo.
Ijapokuwa Ushuja wao kwa kuuwa watu, waasi wa M23 wanaalikwa kulinda watu na Maisha yao kila Leo, bila uregevu na kuondoka piya juu ya udongo wa DRC, ambayo wanakuwa wakitawala bila sababu.
Ni Vema kujuwa kuwa, Maisha ya Mtu inakuwa na lengo Zaidi ya yote.