Ferran Torres ndiye aliyeipa Hispania ushindi huo muhimu kwa kufunga dakika ya 106. Shambulio hilo lilianzishwa na Lamine Yamal, aliyempa Nico Williams mpira kabla ya Williams kumtengenezea Torres nafasi ya kufunga bao la ushindi.
Katika fainali hiyo, Hispania ilitawala kwa kiasi kikubwa. Yamal, Mikel Oyarzabal, Álex Baena na Dani Olmo wote walijaribu kuifungia timu yao, lakini kipa wa Argentina alikuwa imara na kuzuia mashambulizi hayo.

Argentina, kwa upande wake, ilipata wakati mgumu kutengeneza nafasi za maana na haikupiga shuti lolote lililolenga lango la Hispania.
Pigo kubwa kwa Albiceleste lilikuja dakika ya 90+3, pale Enzo Fernández alipopewa kadi yake ya pili ya njano na kutolewa nje. Argentina ililazimika kucheza muda wa nyongezo ikiwa na wachezaji 10, hali iliyowapa Hispania nafasi zaidi ya kutawala mchezo.
Kwa ushindi huo, Hispania sasa ina mataji mawili ya Kombe la Dunia na imeinyang’anya Argentina taji hilo. Pia ni ushindi mkubwa kwa kizazi kipya cha La Roja kinachoongozwa na Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 18, ambaye ameonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya.
Mwamuzi wa fainali alikuwa Slavko Vinčić wa Slovenia.





























