Katika taarifa rasmi N°401/BUR/M.BKV/1130/2026 iliyosainiwa Septemba 12, Meya wa jiji, Nicolas Kyalangalilwa Mulondani, anatangaza kuwa shughuli za shule, biashara na kijamii na kiuchumi – shule, maduka, masoko na maduka makubwa hazitaanza hadi saa 6 za mchana (12h00).
Hatua hii, kama hati inavyoeleza, inafuatia taarifa ya Katibu Mkuu wa AFC-M23 iliyotangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa kumbukumbu ya wahanga wa moto uliotokea Septemba 10, 2026 huko Bukavu.
Hatua hii inalenga kuruhusu wakazi wa jiji kuonyesha huruma na mshikamano wao kwa familia za wahanga katika kipindi hiki kigumu cha maumivu”, anaeleza Meya.

Raia wa kwanza wa jiji anawaalika ma-Bourgmestre, viongozi wa msingi, wakuu wa shule na wafanyabiashara kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya utekelezaji madhubuti wa taarifa hii.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, moto wa Septemba 10 katika mtaa wa Cimpunda ulisababisha uharibifu mkubwa wa mali na vifo kadhaa, katika jiji ambalo tayari limekumbwa katika miezi ya hivi karibuni na mfululizo wa moto ya kuua.
Bukavu iko chini ya utawala (AFC/M23) tangu Februari 2025, katika muktadha wa mzo wa kiusalama na kibinadamu unaoendelea mashariki mwa DRC.




























