Sheria hiyo mpya inalenga kuondoa muda wa kisheria wa kufungua mashtaka kwa makosa ya kingono dhidi ya watoto. Hii ina maana kuwa waathiriwa wataweza kufungua kesi hata baada ya kupita miaka mingi tangu tukio lilipotokea.
Mswada huo pia unapendekeza kuanzishwa kwa orodha ya kitaifa ya watu wanaoshukiwa au waliotiwa hatiani kwa makosa ya kingono dhidi ya watoto. Aidha, unaleta “amri ya ulinzi” inayomruhusu mwendesha mashitaka kuchukua hatua za haraka za kumlinda mtoto mara tu tukio linaporipotiwa.
Hata hivyo, kupitishwa kwa sheria hiyo kumeibua pingamizi kutoka kwa baadhi ya mashirika na vyama vya upinzani. Wanasema kuwa sheria hiyo haitafanikiwa kikamilifu bila rasilimali za kutosha.
Kwa mujibu wao, kuna takribani nafasi 30,000 za kazi ambazo hazijajazwa katika idara za ulinzi wa watoto nchini humo, huku mswada huo ukitajwa kutokuwa na mpango wa wazi wa kuongeza bajeti au wafanyakazi.
Baada ya kupitishwa na Bunge la Kitaifa, mswada huo sasa utapelekwa katika Seneti kwa usomaji wa pili.





























