Sekta ya habari nchini congo imepatwa na msiba mkubwa usio na kifani. Wanahabari watatu wa Kongo wamefariki dunia ndani ya masaa 48 pekee, kati ya siku ya Yumapili tarehe 7 na Yumanne tarehe 8 Mwezi wa Tisa 2026, kati ya Goma, makao makuu ya Kivu Kaskazini, na Kinshasa, mji mkuu wa RDC.
Ndugu wetu wa kazi Shelo, mwanahabari wa michezo, mpiga picha na mpiga video anayejulikana sana kwenye viwanja vya michezo mjini Goma, amefariki siku hii ya Yumanne tarehe 8 Mwezi wa Tisa 2026 mjini Goma, katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Akiwa mtu wa muhimu sana kwenye viwanja vya mpira wa miguu mjini Goma, amefanya kazi kwa miaka mingi akitangaza mashindano ya eneo hilo kama mwanahabari, mpiga picha na mpiga video, akifanya kazi na vyombo vingi vya habari na mashirika ya michezo ya mji huo.
Sababu za kifo chake bado hazijatangazwa rasmi na familia yake. Kuondoka kwake kumeleta huzuni kubwa kwa jamii ya wanahabari na wadau wa michezo mjini Goma.
Kinshasa: Wenzetu wengine wawili walifariki jana, tarehe 7 Mwezi wa Tisa 2026
Wakati huo huo, wenzetu wengine wawili walipoteza maisha yao jana Yumatatu tarehe 7 Mwezi wa Tisa mjini Kinshasa: Ouriel Mangitukwa Lukombo wa chombo cha habari Dépêche.cd
Mwanahabari Ouriel Mangitukwa Lukombo, mwanachama wa waandishi wa Dépêche.cd, alifariki usiku wa tarehe 6 kuamkia tarehe 7 Mwezi wa Tisa kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea kwenye saut-de-mouton ya rond-point Socimat, katika eneo la Gombe mjini Kinshasa. Gari lake liligonga kizuizi cha barabara.
Mwili wake ulipelekwa kwenye hifadhi ya maiti ya Camp Tshatshi.
Baada ya kupita Kinshasa Times na Idara ya Mawasiliano ya Wizara ya Elimu ya Taifa, alielezewa kuwa mwanahabari mwenye bidii na aliyejitolea.
Guy Kitoko Aloma (RTNC)
Mpiga picha wa video Guy Kitoko Aloma, wa Shirika la Utangazaji la Taifa la congo (RTNC), alifariki pia katika moto mkubwa uliotokea kwenye ukumbi wa sherehe wa Panacée mjini Lingwala, Kinshasa, usiku wa tarehe 5 kuamkia tarehe 6 Mwezi wa Tisa. Kulingana na Muungano wa Kitaifa wa Wapiga Picha wa Video wa Kongo (UNCC), alikuwa eneo hilo kama mwalikwa.
Akiwa mwanachama kamili na mwanachama wa Kamati ya Wazee ya UNCC, kifo chake kinaongeza idadi ya waliofariki kufikia watu 22 katika msiba huo.
Msiba huu mkubwa unatokea siku ile ile ambayo ulimwengu unaadhimisha, tarehe hii 8 Mwezi wa Tisa, Siku ya Kitaifa ya Ushikamano wa Wanahabari.
UNPC, AJSC, UNCC na sekta nzima ya habari wanatoa mkono wa pole kwa familia za kibiolojia na za kikazi za waliotutoka.
Pumzikeni kwa amani wenzetu.





























