Akizungumza katika kikao cha hadhara kuhusu umri unaofaa wa kuanzisha IA katika elimu, waziri huyo alikadiria kuwa hakuna umri mmoja unaotumiwa kwa matumizi yote. Kwa DRC, mtazamo unaopendekezwa unategemea utekelezaji wa hatua tatu: kuelewa teknolojia, kujifunza kuzitumia chini ya usimamizi, kisha kupata uhuru kwa taratibu katika mazingira ya ulinzi.
Mwalimu katikati, sio kanuni za kompyuta (algoriti)

Waziri alisisitiza nafasi isiyoweza kubadilishwa ya walimu mkabala na mabadiliko ya kiteknolojia.
« IA inaweza kusaidia kazi ya mwalimu; haipaswi kuchukua nafasi yake, wala kumweka mtoto pekee yake mbele ya mtandao wa mazungumzo (agent conversationnel) », alisema Raïssa Malu.
Alikumbusha pia katika fursa hiyo pendekezo rasmi la UNESCO la kuruhusu matumizi ya kujitegemea ya zana za IA kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 13.
Vizingiti vinne kuu kwa DRC
Ili kudhibiti mabadiliko haya katika mfumo wa elimu wa congo, Waziri wa Jimbo aliweka maagizo manne ya msingi:
Ulinzi wa taarifa binafsi na za kishule za wanafunzi;
– Ufikiaji unaofaa kulingana na umri na mahitaji ya kuelimisha;
– Uchujaji wa maudhui ukiwa na ulinzi ulioimarishwa kwa watoto;
-Usimamizi wa mwanadamu, ukihakikisha kuwa hakuna IA inayoweza kuamua pekee yake kuhusu tathmini au uelekezo wa mwanafunzi.





























