Akiwa amekwama katika eneo linalotawaliwa na waasi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini wakati wa uteuzi huo, msomi huyo anaeleza kuwa hakuweza kupinga uamuzi huo papo hapo kwa sababu maisha na usalama wake vilikuwa hatarini.
Akiwa salama sasa nchini Uswisi, anakataa kabisa uamuzi huo wa kulazimishwa na anaiomba serkali ya Kinshasa kuzingatia mazingira ya hofu na vitisho aliyokuwa akiishi chini yake.
Kati ya shurti za kisilaha na haki za kazi
Jambo hili linadhihirisha tena hatari wanayokumbana nayo wasomi na raia waliotekwa katika maeneo ya mgogoro kwenye
Ukanda wa Maziwa Makuu.
Katika ombi lake alilotuma kwa mamlaka husika, mtafiti huyo ametoa maombi makuu matatu:
-Kutambuliwa rasmi kwa hali ya shuruti na shinikizo iliyozunguka uteuzi wake uliofanywa na viongozi wa M23.
-Kurekebishwa mara moja kwa hali yake ya kiutawala ndani ya mfumo wa elimu ya juu nchini congo.
– Kurejeshwa na kulipwa kwa madai ya mishahara yake, iliyositishwa kufuatia tukio hilo.
Kwa kuwasilisha swala hili kutoka Barani Ulaya, Profesa Bengea Matchozi Déo anakusudia kuhamasisha jamii ya kimataifa kuhusu vitisho vinavyofanywa na makundi ya silaha dhidi ya wasomi na watumishi wa serikali waliobaki katika maeneo yanayotawaliwa na waasi.





























